Alhamisi Septemba 22 2016
Obama amesema bara la Afrika linakuwa haraka kiuchumi
Rais Obama akizungumza kwenye mkutano wa biashara kati ya | Marekani na Afrika huko New York, Sept. 21, 2016. |
Huku kukiwa na migogoro, umaskini na magonjwa barani Afrika, Rais wa Marekani Barack Obama alisema njia pana kwa bara hilo haijakosewa. Bara la Afrika linapiga hatua.Kwenye mkutano wa biashara kati ya Marekani na bara la Afrika huko New York, Obama alisema Afrika ni makazi ya uchumi unaokuwa haraka duniani na daraja la kati linatarajiwa kukua kwa zaidi ya wateja bilioni moja. Kampuni za mawasiliano Afrika na zinaendeshwa na vijana wadogo duniani.
Mmojawapo wa vijana hao wa kiafrika, Fraances Udukwu kutoka Nigeria
aliiambia Sauti ya Amerika-VOA kile anachotumaini kuelezea wakati wa
muda wake wa kushikilia taji kwa mwaka mmoja la Miss Africa USA, mbali
ya kutangaza urembo, kipaji na uwezo wa wanawake wa Afrika katika
Diaspora, alisema kwamba anaona Miss Africa USA kama fursa ya kuelezea
mahala alipotoka, ambapo ni makazi ya bara la Afrika. Lakini pia
kuheshimu mahala ninapoishi ambapo ni hapa nchini Marekani.
Udukwu anasoma chuo kikuu cha Temple huko Philadelphia katika masomo ya afya ya jamii. Akiwa na umri wa miaka 26 hivi karibuni alianzisha shirika lisilo la kiserikali la The Lead Girl Foundation, ili kuwasaidia wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kimaisha kupitia ujasiriamali na mafunzo ya ufundi.
Udukwu anasoma chuo kikuu cha Temple huko Philadelphia katika masomo ya afya ya jamii. Akiwa na umri wa miaka 26 hivi karibuni alianzisha shirika lisilo la kiserikali la The Lead Girl Foundation, ili kuwasaidia wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kimaisha kupitia ujasiriamali na mafunzo ya ufundi.
Rejea hapa
Alhamisi Septemba 22 2016
Chips yai adui yako
MAMBO vipi wadau. Wakati nasoma tahadhari aliyotoa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuhusu madhara ya chips mayai nilikumbuka maswali niliyoyaona katika mtandao wa intaneti kuhusu chakula hicho maarufu nchini.
Miongoni mwa maswali hayo ni; nani aliyekuja na ubunifu wa chips mayai? Kwa nini chakula hicho kimekuwa maarufu sana? Pamoja na kutoa ajira nyingi kwa vijana ni fursa gani zaidi zimetengenezwa na chips mayai kwa jamii? Nini faida ya chips mayai mwilini? Nini madhara ya chips mayai? Kwa nini watu hupenda zaidi zege lililotayarishwa na Wapemba?
Kwa nini wapika chips wengi ni wanaume? Na kwa nini zege likipikwa na mwanamke linadoda? Waziri Ummy amewataka Watanzania waache kula chipsi mayai kila siku kwa kuwa ni hatari kwa kiafya. Mabachela na wanafunzi vyuoni mpo?
Ametoa angalizo hilo mjini Dodoma wakati wa kufunga mafunzo ya wasimamizi na wadadisi wa utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi Tanzania wa mwaka 2016.
Amesema wananchi wale mlo bora wenye tija katika miili na si chipsi mayai a.k.a zege. Kuna wenye mtazamo tofauti na wa Waziri Ummy kwa maelezo kwamba, wanaotaja madhara ya ‘viepe yai’ waeleze pia faida ya chakula hicho pendwa.
Kudharau hatari ya chips mayai hakubadili ukweli kuwa, chakula hicho kina mafuta mengi na inadaiwa kuwa ni miongoini mwa vyakula vinavyopikwa kwa zaidi ya nyuzi joto 300.
Unapokula chips mayai tambua kuwa unaongeza kiasi kikubwa cha mafuta ambayo ni hatari kwa mwili wako na kama hufanyi mazoezi unakaribisha matatizo ya moyo hasa yanayotokana na kuziba kwa mirija.
Inadaiwa kwamba, mwili wa binadamu hautupi kinachofaa, kama hakitumiki huhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye na ndiyo maana unapokula vyakula vyenye mafuta mengi unaongezeka unene na uzito.
Unene ni chanzo cha magonjwa mengi kwa sababu ya wingi wa mafuta mwilini unaosababisha kuziba kwa njia za kusafirisha damu. Hali hiyo inasababisha nguvu ya ziada itumike kusukuma damu hiyo ili isambae mwilini hivyo kuongeza mapigo ya moyo. Mapigo ya moyo yanapoongezeka yana madhara na pia yanapopungua sana ni hatari.
Ingawa wengi wanapenda kula chips kwa sababu mbalimbali ukiwemo urahisi wa kuzipata, bei na mtazamo kwamba hazikinaishi, si busara kudharau tahadhari inayotolewa zikiwemo taarifa zinazodai kuwa, chakula hicho ni chanzo vifo vya ghafla, kinachangia kupunguza nguvu za kiume na kinaongeza kasi ya mwanadamu kuzeeka. Wapenda chips wanapaswa kubadilika, wasithamini utamu kuliko usalama wa afya zao.
Huhitaji elimu ya udaktari kufahamu kwamba, matunda na mboga mboga ni muhimu mwilini na si lazima uwe na Shahada kutambua kwamba, miongoni mwa maadui wakubwa kwa afya zetu ni sisi wenyewe. Siku njema.
Imeandikwa na Basil , rejea hapa.
Alhamisi Septemba 22 2016
Wanaume nao hupata saratani ya matiti
SARATANI ni chembechembe zisizokuwa za kawaida zinazozaliana kwa haraka kwenye mwili wa binadamu bila mpangilio maalumu.
Tafiti zinaonesha kwamba hakuna sababu maalumu inayojulikana
kusababisha saratani, ila kuna vichocheo vinavyoweza kusababisha
saratani. Vichocheo hivyo viko katika makundi mbalimbali kama vile
matumizi ya kemikali, uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe kupita kiasi,
utumiaji wa vyakula vyenye mafuta kupita kiasi, unene kupita kiasi pia
kutofanya mazoezi kwa watu wanene.Ni ukweli usiopingika kuwa saratani imekuwa chanzo cha magonjwa na vifo. Inakadiriwa kuwa takribani wagonjwa wapya 45,000 hugundulika kila mwaka wakiwa na saratani za aina mbalimbali kutokana na kuchelewa kugundulika mapema. Aidha, ugonjwa wa saratani umekuwa tishio katika nchi za Afrika zilizo chini ya Jangwa la Sahara. Hapa nchini, tafiti za kitaalamu kuhusu afya ya binadamu zinaonesha miongoni mwa magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo na upotevu wa nguvu kazi.
Zipo saratani za aina mbalimbali. Nazo ni saratani ya shingo ya kizazi, matiti, utumbo mpana na saratani ya tezi dume. Katika mkutano wa 10 wa kufanya mapitio juu ya hatua zilizochukuliwa na nchi za Afrika kukabiliana na saratani, jijini Addis Ababa Ethiopia, inaelezwa hali halisi ya maradhi haya. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alihudhuria mkutano huo, takribani wagonjwa wapya 45,000 wa saratani wanagundulika kila mwaka.
Kati yao, asilimia 38 ni wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake, asilimia 14 saratani ya ngozi, asilimia 10 saratani ya matiti na asilimia nne ni ya tezi dume. Aidha, takribani watu 35,000 hufariki kila mwaka kutokana na saratani. Ummy anaeleza kuwa kutokana na ukubwa wa tatizo, serikali imepitisha sera za kitaifa na miongozo mbalimbali ya kukabili maradhi haya. Aidha, inatoa elimu kwa jamii na watoa huduma za afya .
Serikali imeanzisha huduma za upimaji wa saratani katika hospitali na vituo vya afya zaidi ya 300 na huduma za tiba kupitia Hospitali ya Saratani ya Ocean Road. Waziri anasema serikali inaendelea kupanua wigo wa matibabu ya saratani katika Hospitali ya Bugando Mwanza na KCMC – Kilimanjaro. Anasema serikali itaanza kutoa chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa watoto wenye umri wa miaka kati ya tisa na 13 kukabiliana na changamoto ya maradhi hayo nchini. Saratani ya shingo ya kizazi inaambukizwa na virusi vinavyojulikana kama Human Papiloma Virus (HPV).
“Tumeamua kuteua kundi la watoto wa rika dogo kwani wengi wao katika umri huo wanakuwa bado hawajaanza kujihusisha na vitendo vya mapenzi,” anasema Waziri Ummy. Katika bajeti ya mwaka 2016/17 Serikali imepanga kuipatia Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kiasi cha Sh bilioni tatu kwa ajili ya ununuzi wa dawa ikilinganishwa na Sh milioni 600 zilizokuwa zimetengwa katika bajeti ya mwaka 2015/16.
Mtafiti na bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya saratani, kutoka Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam, Dk Walter Kweka anaeleza saratani kuwa miongoni mwa majanga yanayonyemelea kila Mtanzania. Anataja ongezeko la ugonjwa huu linachangiwa na sababu za mazingira, vyakula, sababu za kurithi na mtindo wa maisha wa watu wengi mijini na vijijini. Dk Kweka anataja aina kuu za saratani zinazoongoza kuathiri maisha ya watu wengi nchini ni ya shingo ya kizazi, tezi dume, utumbo mpana na saratani ya matiti kwa wanaume na wanawake.
Saratani shingo ya kizazi Dk Kweka anasema miongoni mwa saratani zote, ya kizazi inaongoza kwa kusababisha vifo kwa wanawake. Wapo wanaokumbwa na ugonjwa huu kwa sababu za kurithi ndani ya koo. Wanawake walioanza kufanya ngono katika umri mdogo na wale wenye mpenzi zaidi ya mmoja, pia ni miongoni mwa waathirika wa ugonjwa huu ambao husababishwa na virusi vijulikanavyo kama Human Papiloma Virus (HPV).
Mwanamume ndiye hubeba virusi hivi ambavyo mwanamke huambukizwa kwa njia ya kujamiiana. Miongoni mwa mambo yanayodhihirisha kuwa mtu ana saratani hii, ni maumivu wakati wa kujamiiana, kutokwa na majimaji yenye harufu mbaya au uchafu usio wa kawaida ukeni. Pia kutokwa na damu kidogo au nyingi ukeni wakati wa kujamiiana au kutokwa damu ukeni kwa wanawake waliokoma hedhi.
Dalili nyingine ni maumivu sehemu ya nyonga au chini ya tumbo, kuvimba kwenye kinena, kutokwa na damu kidogo au nyingi ukeni wakati ambao mwanamke hayuko kwenye hedhi. Dk Kweka anasema zaidi ya asilimia 80 ya wanawake wanaougua saratani hiyo hufariki ndani ya miaka mitano kwa kuwa hufika hospitali wakiwa wamechelewa. “Upimaji wa saratani ukifanyika kwa ufasaha, unasaidia kugundua tatizo mapema hivyo mhusika hupata fursa ya kutibiwa mapewa, ni vyema wanawake wakajenga tabia ya kufanya uchunguzi angalau mara moja kwa mwaka,” anasisitiza Dk Kweka.
Tanzania inakadiriwa kuwa zaidi ya wanawake milioni 14 walio katika umri wa kuzaa kuanzia miaka 18 hadi 45 wako kwenye hatari kubwa ya kupata saratani ya shingo ya kizazi. Takwimu za utafiti zinaonesha, wanawake wa Kitanzania wanaopata saratani hii kwa mwaka ni 7,304 na wanaofariki kutokana na saratani hii ni 4,216. Sababu inayochangia vifo ni uwezo mdogo wa kumudu gharama za matibabu, kupuuzia kufanya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali zinapojitokeza dalili za awali.
Wengine hufika hospitalini tatizo likiwa kubwa na baadhi yao hubakia nyumbani wakiamini kuwa wamefanyiwa vitendo vya kishirikina. Saratani hii hujitokeza wakati ikiwa imesambaa na ni vigumu kuitambua mpaka vipimo vya kitaalamu vinapofanyika. Ikigundulika, tiba hufanyika kupitia upasuaji kuondoa seli zote zilizoathirika au kuondoa kizazi kuokoa maisha ya mama. Saratani ya matiti Inaongoza kushambulia wanawake walio katika umri wa kuzaa; miaka 18 hadi miaka 45.
Katika Afrika Mashariki, inakadiriwa wagonjwa wapya wa saratani ya matiti kwa mwaka wanafikia 18,000. Kati yao, 10,000 hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huo. Dalili za saratani ya matiti ni uvimbe mgumu kwenye titi au kwapani, kupata mabadiliko ya umbo au ukubwa wa titi. Pia kunakuwapo mabadiliko ya rangi ya ngozi ya titi ambayo huonekana na mikunjo kama sehemu ya nje ya ganda la chungwa. Dalili nyingine ni mwanamke kuwa na chuchu zilizoingia ndani na wakati mwingine zinazotoa majimaji machafu au damu.
Mwaka 2008 inakadiriwa kuwa kulikuwa na zaidi ya wagonjwa wapya 2,500 waliogunduliwa kuwa na saratani ya matiti. Kati ya hao, wagonjwa 300 ndiyo walipata tiba katika ya Hospitali ya Ocen Road. Zaidi ya asilimia 90.7 ya wagonjwa wanaofika katika Hospitali ya Ocean Road wanakuwa wamechelewa na ugonjwa unakuwa katika hatua ya juu. Dk Kweka anasisitiza jamii kuchukua hadhari mapema kujikinga na maradhi hayo kuliko tiba.
“Mgonjwa anapochelewa kufika hospitalini na hali yake ikawa mbaya, matibabu yake ni ghali na yanaambatana na uvunaji au uondoaji wa viungo,” anasema. Mathalani, mgonjwa mwenye saratani ya matiti, hufanyiwa upasuaji maalumu kuondoa uvimbe ulioko ndani ya titi na iwapo athari ni kubwa, titi lote huondolewa au huvunwa. Mgonjwa aliyevunwa titi moja huwekwa chini ya uangalizi maalumu wa kitaalamu kwa muda wa miaka mitano akifanyiwa uchunguzi kuangalia kama ana maambukizi kwenye titi la pili.
Anasema zaidi ya watu wapya milioni 10 hufanyiwa uchunguzi kubaini kama wamepata ugonjwa wa saratani kila mwaka duniani. Pia watu milioni sita hupoteza maisha kutokana na ugonjwa huo na wengine milioni 24.4 kwa mujibu wa takwimu zilizopo wanaishi na saratani.
Wanaume na matiti
Dk Kweka anasema wanaume 1,000 wanaoonwa kwa mwaka katika Hospitali ya TMJ na kufanyiwa uchunguzi wa saratani, asilimia mbili hadi saba hugunduliwa kuwa na saratani ya matiti. Anasema, kwa wanaume hali hiyo hujitokeza katika umri mkubwa kidogo tofauti na akina mama ambao huanza kupata athari kuanzia umri wa miaka 20 mpaka 50. Saratani kwa wanaume hujitokeza kuanzia miaka 45 na kuendelea. Mara nyingi wanaume hupata hali hiyo kutokana na kurithi.
Tezi dume Saratani ya tezi dume ni aina nyingine inayoshambulia wanaume wenye umri kuanzia miaka 50 mpaka 70. Chanzo kikubwa cha saratani hii ni ulaji wa muda mrefu wa vyakula vyenye mafuta mengi, nyama nyekundu, pamoja na sababu za kurithi. Wanaume zaidi ya 1,200 hugundulika kuwa na saratani ya tezi dume kila mwaka. Anasema utafiti wa mwaka 2010 katika Hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro ulionesha asilimia 8.9 ya wagonjwa waliofika kufanyiwa uchunguzi wa tatizo la njia ya mkojo waligundulika kuwa na saratani hiyo.
Utafiti kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili unaonesha asilimia 38 ya wanaume wenye tatizo la kukua kwa tezi dume walikutwa na saratani hiyo na walikuwa na umri kati ya miaka 60 na 70. Aidha, wanaume waliokuwa na saratani hii walio na umri chini ya miaka 60 walikuwa asilimia 7.2. Kweka anatoa angalizo akisema, wananchi wengi huchukulia ugonjwa wa saratani kama jambo la kawaida. Anasema wakati mwingine hupuuzia ushauri wanaopewa na wataalamu kuhusu njia sahihi za kujikinga na tiba ya ugonjwa huo.
Anasema hakuna ukoo wa Mtanzania ambao haujawahi kuguswa na tatizo la ugonjwa wa saratani. Anasisitiza juhudi za pamoja zinahitajika kukabili ugonjwa huu. Anahadharisha juu ya matumizi ya sigara, unywaji wa pombe kupita kiasi, matumizi ya kemikali au homoni hasa kwa wanawake wanaolenga kubadili sura na mwonekano wa maumbo ya miili yao. Anasema mambo haya ni miongoni mwa sababu zinachangia kukithiri kwa ugonjwa huu miongoni mwa jamii.
Pia ulaji wa mara kwa mara wa vyakula kama vile chipsi kuku, mayai ya kuku wa kisasa, ulaji wa soseji, baga, matumizi ya kiwango kikubwa cha nyama nyekundu huweka wahusika katika mazingira hatarishi ya kupata ugonjwa huu. “Utafiti nilioufanya kama daktari bingwa mwaka 2013 na kuuchapisha kwenye majarida mbalimbali ya kisayansi, unaonesha kuwa matumizi ya vyakula aina ya chipsi kuku, mayai ya kisasa, soseji ulaji wa baga ni chanzo kikubwa cha watu kupata saratani ya utumbo mpana nchini,” anasisitiza Dk Kweka.
Anasema sababu ya mtu kuwa na umri mkubwa sambamba na ulaji mbaya wa vyakula vyenye kemikali pamoja na tabia kutokwenda hospitalini kupima afya mara kwa mara, imechangia kukuza tatizo miongoni mwa jamii. Mabadiliko ya mtindo wa maisha yameliingiza kundi kubwa la watu kupata saratani. Mtindo wa maisha kuanzia ngazi ya familia umesababisha kila mtu kuwa mwathirika.
Anashutumu watu kuiga umagharibi na kuacha kula vyakula vya asili kama vile ugali wa dona, mboga za majani kama vile matembele, bamia na bilinganya. Asasi isiyo ya kiserikali ya Social Outreach Initiative ( TASOI) ambayo inajishughulisha na utoaji wa elimu na utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii katika masuala ya afya na uchumi, inasisitiza juu ya ulaji.
Katibu Mtendaji wa TASOI, Belinda Mlingo anaeleza kuwa Watanzania walio wengi hawana uelewa wa kutosha juu ya chanzo, madhara, kinga na tiba sahihi ya saratani. Anasema wakati umefika kwa Watanzania kuamka na kuchukua hadhari dhidi ya ugonjwa huo. Belinda anasisitiza wananchi kuchunguza afya mara kwa mara wakizingatia kwamba, gharama za kutibu saratani ni kubwa na wanaoweza kuzimudu ni wachache.
Rejea Habari Leo. Gwiji la habari Tanzania.
Alhamisi Septemba 22 2016
Umemejua, nishati inayopaswa kuangaliwa vyema zaidi na serikali
MOJA ya vitu vinavyoaminika kwamba vitarahisisha maendeleo yetu ni upatikanaji wa nishati iliyo bora na rahisi.Sekta ndogo ya nishati mbadala kama vile umemejua (sola), gesi itokanayo na kinyesi cha wanyama, umeme utokanao na upepo au mawimbi na matumizi endelevu zaidi ya mimea katika kuzalisha nishati ina fursa kubwa ya kuchangia maendeleo endelevu mijini na vijijini. Wakati serikali ikijikita katika kusambaza umeme nchini na hususan vijijini, sekta binafsi zimekuwa haziko nyuma pia katika kusaidia jukumu hilo la kusambaza na kushauri matumizi ya nishati mbadala kwa ajili ya kuleta chachu ya maendeleo nchini.
Taasisi ya IMED ni moja ya zilizo mstari wa mbele katika kutoa huduma za kuendeleza ujasiriamali pamoja na ushauri kwenye masuala mbalimbali lakini pia inajihusisha na nishati mbadala. Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Dk Donath Olomi anasema Imed inayo Kiatamishi cha Ujasiriamali wa Nishati Endelevu (Tarebi), ambacho kinajihusisha na umeme jua, mkaa bora, kuni bora, bayogesi, majiko sanifu na uzalishaji wa umeme kwa kutumia mashudu ya kilimo na mimea kama pumba za mpunga.
Vile vile anasema kuna mjumuiko wa wadau na wataalamu wa vifaa vya umemejua, ambao wanajihusisha pia na kujadili sera na kuishauri serikali pamoja na kusimamia ubora wa huduma katika sekta hiyo ndogo ya nishati. Mjumuiko huu unaitwa Solar Community of Practice (COP – Solar). Dk Olomi anasema mjumuiko huo wa wadau hukutana mara kwa mara ili kujadili changamoto zilizopo na kuangalia jinsi gani ya kuziondoa pamoja na kubadilishana uzoefu na kisha kuja na njia mbalimbali za kuondoa hizo changamoto.
Anasema mjumuiko huo wa wadau hivi sasa wanafanyia kazi ya kuziondoa sokoni bidhaa za umemejua zisizokuwa na ubora, yaani bidhaa feki. Mkurugenzi wa Uhandisi kutoka Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), ambaye pia ni mdau wa nishati jadidifu, Dk Lugano Wilson, anasema wao ni miongoni mwa wanajumuiko la wadau wanaokutana ili kujadili changamoto na fursa zilizopo kwenye tasnia ya nishati mbadala.
“Katika kukutana kwetu, tunajifunza jinsi gani ya kutatua matatizo kuhusiana na nishati jadidifu hususan umemejua,” anasema Dk Wilson. Anasema umoja huo ulianzishwa kwa sababu wadau pamoja na wafanyabiashara wa umemejua wamekuwa na matatizo yanayowakabili, hivyo wameona peke yao hawawezi kutatua ila kwa kupitia umoja wao inakuwa rahisi. Anasema nishati jadidifu ndio mwelekeo wa dunia kwa sasa kwa vile ni nishati endelevu zinazopunguza uharibifu wa mazingira.
“Kule Ulaya wana mipango maalumu ya kuendeleza nishati jadidifu lakini hapa kwetu utaratibu bado haupo. Wenzetu wameweka mfumo ambao unafanya gharama za kumiliki nishati jadidifu kuwa nafuu. “Mji wa Stockhom, Sweden, kwa mfano, halmashauri imesema teksi inayoruhusiwa kwenda uwanja wa ndege wa Arlanda ni ile tu inayotumia nishati jadidifu, vile vile mabasi yao yote yanayosafirisha abiria hutakiwa kutumia nishati hiyo,” anasema.
Anasema wadau wameona wachukue umuhimu wa pekee katika suala la umemejua kwa kuwa sasa kuna wadau wengi hivyo ni sekta ambayo inakua. Anakiri kwamba pamoja na sekta hiyo kukua yameanza kujitokeza matatizo ya udanganyifu wa ubora na kwamba hata utaalamu wa ufungaji wa huduma hiyo nao umekuwa changamoto. Vile vile anasema bei ya vifaa vya umemejua nayo imekuwa changamoto pamoja na elimu ndogo ya watumiaji.
Anasisitiza kuwa athari za ubora mdogo wa vifaa vya umemejua inaua soko la wafanyabiashara wa nishati hiyo na pia inakosesha imani ya mtumiaji. Anafafanua kwamba katika kila paneli ina watts zake, na kwamba itakapokaa mahala hata kwa miaka minne ubora unatakiwa kuwa ule ule wa mwanzo kama sio feki. Anasema utaalamu pia unatakiwa katika ufungaji kwani paneli ya watt 80, kwa mfano, ikifungwa vibaya itatoa umeme mdogo, chini ya watt 80.
“Ili paneli ifanye kazi yake vizuri lazima uiegeshwe ipate mwanga wa kutosha kutoka kwenye jua. Wengi hapo wanakosea badala ya kuegesha kuelekea jua wanafunga tofauti,” anasema. Anasema kwa sasa bei za vifaa vya umemejua viko juu lakini anaamini tafiti za kitaalamu zikifanyika zina nafasi kubwa ya kupunguza bei. “Lakini kwa sasa njia ya mkato ni kwa kuzungumza na serikali kuhusu kupunguza kodi ya vifaa vya umemejua,”
Rejea Habari Leo. Gwiji la habari Tanzania.
KILIMO MJINI
UKULIMA KWA WENGI NI KAZI YA MASHAMBANI, NA HATA LABDA YA WATU AMBAO HAWAJASOMA. LAKINI WAJUA KUNA WATU WANAOPATA FEDHA KIASI CHA HAJA, KUPITIA KILIMO AMBACHO HUKUZWA NDANI YA BANDA KITALU, AL-MAARUFU GREENHOUSE ,HASA MIJINI. MWANAHABARI WETU HUBBAH ABDI, ALIKUKUTANA NA DANIEL KATHUKU, AMBAYE HUTENGEZA BANDA KITALU AU KIVUNGULIO, KWA KUTUMIA FITO BADALA YA CHUMA, KWA WALE WASIO NA UWEZO, WA KUNUNUA CHUMA
HOTUBA YA MH:MWIGULU NCHEMBA YA BAJETI YA WIZARA YA KILIMO,MIFUGO NA UVUVI 2016/2017
Pakua hotuba ya kusoma hapa { Pakua}