Ili kuimarisha umoja na mshikamano unaoendelea baina ya watanzania, inahitajika kwa kila mwenye jambo lolote halali la kimanufaa ,ampatie mwenzake walau kiasi kidogo.Na hii siyo katika vitu tu,bali hata elimu ya ujuzi.Watanzania hatutakiwi kuwa wabinafsi baina yetu kimaendeleo.Mbinu kubwa itakayotuletea maendeleo watanzania ,ni kuukataa na kuupiga vita ujinga.
Ni vipi tutaupiga vita ujinga; ni kuacha ubinafsi wa ujuzi na mali baina yetu.Kutokana na hivyo basi, nimeonelea kuuweka ukurasa huu ili kutoa kile nilicho nacho katika ujuzi ,ili kila mwenye kushawishika afanye maamuzi.
JINSI YA KULIMA UYOGA
Tafadhali tushirikiane mwanzo mpaka mwisho kabla ya kukata shauri la kuingia shambani,