UYAOGA CHAZA (OYSTER MUSHROOM)
Aina hii ya uyoga umeitwa jina hili
kwa kuwa una muonekano wa samaki aitwaye
Chaza (Oyster Fish), Aina hii ya uyoga mar azote hupatiakana ukiwa na moja kati
ya aina mbili za rangi, nyeupe na chanikiwiti (greyish).Aina hii ya uyoga pia
hunukia kama harufu ya samaki chaza.
Tofauti na aina zingine za uyoga, uyoga
wa oyster,hutoa shina imara ambalo huishia na kofia yenye muonekano mfano wa
feni ambalo hukuwa mpaka kufikia upana kati ya Sentimeta 5 mpaka 25.
FAIDA ZA UYOGA KWA MLAJI
Wataalam wa lishe wameuweka uyoga katika kundi la mboga za majani,lakini
kiuhalisia uyoga unapatikana katika kundi la fungi, utofauti huu wa uyoga
kutofautiana na mboga za majani,umeufanya uyoga uwe na faida nyingi zaidi za
kiafya kuliko mboga za majani.
Katika mwili wa mlaji,Uyoga una
faida zifuatazo:-
1. Hupunguza
mafuta yaliyozidi mwilini(cholesterol levels).
Uyoga huupatia mwili protini ya kutosha na kuwa hauna
virutubisho vya mafuta aina ya Kolestro na fat.Wingi wa protini iliopo katika
uyoga husaidia kuyaunguza mafuta ya kolestro yaliyotengenezwa na mwili kutokana
na vyakula vya mafuta na kuyaondoa,hatimaye
kuweka uwiano sawa wa mafuta yanayohitajika katika mwili.
2. Ni kinga
dhidi ya Anemia.
Mgonjwa wa anemia hukumbwa na hatari kubwa ya kuwa kiasi cha
chini cha madinichuma katika damu yake,kiasi ambacho hupelekea matatizo ya
udhaifu wa kazi za kichwa,kupungua kwa kazi za neva za fahamu,na matito ya
umengenywaji wa chakula.
Uyoga ni chanzo kizuri cha madinichuma ,asilimia kubwa ya
madinichuma yanayosharabiwa na mwili ,husisimua hutzalishaji wa seli nyekundu
za damu hatimaye kumfanya mtu awe na afya nzuri na mwili kuwa katika hali yake
ya asili.
3. Hukinga na
kuondoa Kansa ya matiti,na kansa ya makende.
Uyoga una uwezo mkubwa wa kukinga maradhi haya kutoka na
kuwa na asidi zinazojulikana kama Beta-Glucans na Linoleic.Asidi ya Linoleic
husaidia sana katika madhara mabaya Zaidi yanayosababishwa na homoni ya ziada
ya estrojeni.Uongezekaji wa homoni hii ya estrojeni kupita kiasi chake ni mmoja
ya sababu za msingi za kansa ya matiti kwa mwanamke aliyesimama kupata siku
zake(Meno pause).
Asidi ya Beta-glucans kwa upande mwingine ,huzuia ukuajia wa
seli za kansa katika tatizo la kansa ya makende.
Chunguzi na majaribio mengi yametuonesha uwezo mkubwa wa
uyoga wa kuondoa vimbe za kansa pindi unapotumika kama tiba.
4. Kinga na
tiba dhidi ya Kisukari.
Uyoga hauna mafuta aina ya fat,wala mafuta aina ya
kolestro.una kiasi kidogo sana cha wanga,una utajiri mkubwa wa protini,vitamini
na madini.Pia una maji mengi na kambakamba(fiber) .Zaidi ya hayo uyoga
umekusanya insulin ya asili na vimeng’enya(enzymes) ambavyo husaidia
kuvunjavunja sukari na wanga katika chakula.Hivyo ni salama sana kwa wagonjwa
wa kisukari.
Mgonjwa wa kisukari hukumbwa na hatari ya maambukizi katika
miiguu au mikono yake.Maambukizi haya hupelekea ngozi za miguu au mikono
kuharibika kwa kutia wekundu,kutoka mabaka au vidonda vikubwa ambavyo ni
hatarishi kwa maisha ya mgonjwa.
Tiba asilia iliyopo katika uyoga husaidia kumuepusha mgonjwa
wa kisukari katika hatari hii.
5. Huleta
afya ya mifupa.
Uyoga una utajiri mkubwa wa Kalisi(Calcium) ambacho ni
kiinilishe muhimu kinachotumika katika
utengenezaji na uimarishaji wa mifupa.Usambazwaji imara wa kalisi katika mwili
hupelekea ukuaji imara wa mwili ,kuondoka kwa maumivu ya viungo na udhaifu wa
mwili ambao husababishwa na ukuaji wa mifupa dhaifu.
6. Huimarisha
Kinga mwili.
Kiinilishe chenye nguvu kilichopo katika uyoga kinachojulika
kwa jina la kitaalam Ergothioneine,ni muhimu sana kwa kupambana na kuvunja nguvu asidi
hatarishi zinazo zalishwa katika mwili ,na pia kupiga jeki mfumo wa ulinzi
katika mwili.
Uyoga una dawa kinga za asili ambazo hufananishwa sawa na
dawa iitwayo Penicillin.Dawa kinga
hii huzuia ukuaji wa vijidudu vya magonjwa na maambukizi ya fangasi.Pia
husaidia kutibu athari za vidonda vya tumbo na kuzuia usambaaji wake na
hatimaye kuviondosha kabisa.
Zingatia : Penicillin – ni dawa inayotokana na uyoga wenyewe.
7.
Hudhibili tatizo la shinikizo la juu la damu.
Katika tafiti za wataalam, zimeonesha kuwa uyoga una
Potassium nyingi ndani yake .Potassium katika damu hufanya kazi ya kutanua
mishipa ya damu(vasodilation) pindi damu nyingi inapotaka kupita haliyakuwa
njia ya mishipa wakati huo ipo katika hali ya wembamba;hivyo hupunguza tatizo
la shinikizo kubwa la damu (high blood pressure).
Patassium pia husaidia utendaji kazi mzur wa ubongo kutokana
na kuwa uongezekaji wa msambao wa damu na oksijeni kutoka kwenye moyo kuelekea katika
ubongo ,husisimua utendaji kazi wa neva za fahamu.Chunguzi za kitaalamu
zimeonesha kuwa uongezekaji wa kiasi cha Potassium mwilini huimarisha maarifa
na uhifadhi wa kumbukumbu.
8. Hupunguza
uzito usio halisia.
Hapa bilashaka kuwa
utaniamini kuwa protini ni mashughuli kwa kupunguza mafuta wilini na
kutengeneza uzito halisia wa mifupa.Ni kweli kabisa ukubali au ukatae ya kwamba
mafuta mengi mwilini yaliyo katika hali ya mgando (yaani fat ) huungua na kuyeyuka ili kumeng’enya protini inayotokana na
vyakula tunavyokula.Hivyo mafuta hupungua kwa kiasi kikubwa mwilini kutokana na
uwepo wa protini.
Kutokana na hivyo basi , Protini ikiambatana na kiasi kizuri cha wanga,bila uwepo wa fat au
kolestro hupelekea mtu kuwa na uzito mdogo unaoendana na mwili wake.
9. Tiba dhidi
ya bakteria na vimbe mbalimbali,
Kutokana na utafiti ,uyoga aina ya Oyster umethibitishwa
kuwa una uwezo wa kutukinga dhidi ya bakteria hatari pia na magonjwa ya
vimbe,kama vile vimbe za tumboni kwa akina mama,na vimbe za kansa.
Viinilishe muhimu vinavyopatikana katika uyoga vikiwemo
protein,kalisi(calcium),aside ya amino,valun ,vitamin C na vingine vingi muhimu
ndivyo ambavyo huupa uyoga wa oyster uwezo wa kukufanya uepukane na matatizo
haya.
10. Huondoa tatizo
la ukosefu wa choo.
Tatizo la kukosa choo ,au kupata choo kigumu,ni ishara
tosha kuwa mlo wako una ukosefu
kiinilishe aina ya faiba ( roughage).Ili kuondokana na tatizo hili,basi
itakulazimu kutumia uyoga aina ya oyster katika mlo wako.
No comments:
Post a Comment