1.
Hutumika kama
mboga:
Hupikwa kama inavyopikwa mboga ya samaki au nyama iliyochemshwa tayari kwa
kuungwa mboga.
2.
Hutumika kama
supu:
Hupikwa kama supu ya kuku mbuzi au ng’ombe
na hutumia kiungo chochote cha supu kama chumvi ,ndimu au pilipili.
VYAKULA VINAVYO ENDANA NA UYOGA KATIKA MLO MMOJA.
MAPISHI
YA CHAI YA MAZIWA , MAANDAZI , UYOGA NA MAYAI .
MAHITAJI
Mandazi,
Uyoga (mashroom kikombe 1 cha chai),
Mayai (eggs 4),
Hoho
(greenpepper 1/4 ya hoho),
Nyanya (fresh tomato 1),
Kitunguu (onion 1/4 ya
kitunguu),
Chumvi (salt),
Mafuta (vegetable oil),
Hiliki nzima (cardamon 4),
Masala ya
chai (tea masala 1 kijiko cha chai),
Pilipili mtama iliyosagwa (ground black
pepper 1/4 ya kijiko cha chai),
Maziwa (fresh milk 1 kikombe cha chai),
Majani ya
chai (tea leaves),
Maji kiasi.,
Sukari (sugar)
MATAYARISHO
Jinsi ya kupika chai
Weka maziwa, maji kiasi,hiliki, masala ya chai, pilipili mtama na majani katika
sufuria. Chemsha kwa muda wa dakika 10 na chai itakuwa tayari.
Jinsi ya kupika
mayai
Weka mafuta kiasi katika fry pan na utie vitunguu, vikaange kidogo kisha
tia nyanya, chumvi na hoho. Pika kwa muda wa dakika 4 kisha tia mayai na
uyaache yaive mpaka yakauke kisha geuza upande wa pili na uyapike mpaka ya ive
kisha ipua.
Jinsi ya kupika uyoga
Weka mafuta kidogo katika fry pan kisha tia
uyoga na chumvi na ukaange mpaka uive katika moto wa wastani. Ukisha iva
breakfast yako itakuwa teyari kwa kuseviwa na kuliwa.
Mapishi tofautiya Uyoga
No comments:
Post a Comment